Personal tools
You are here: Home Books Tamthilia Mbili za Kifaransa

Tamthilia Mbili za Kifaransa

by Victor Hugo, Jean-Luc Luc Lagarce edited by Marcel Kalunga Mwela

Professor Marcel Kalunga Mwela-Ubi anatokea Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo na tafsiri hizi zilishinda na kupewa tuzo katika mashindano ya kutafsiri tamthilia za Kifaransa katika Kiswahili. Kwa jinsi maandiko yenyewe yalivyo na mvuto mkubwa, baada ya kusoma kurasa chache na kuzoea matumizi ya Kiswahili cha Congo (Kingwana), msomaji atazama katika uhondo wa ucheshi wa tamthilia hizi na kugundua kuwa, kumbe si lazima, waandishi wote watumie Kiswahili sanifu. Professor Kalunga Mwela-Ubi anaandika hivi kuhusu “Michezo ya Mfalme”:

Katika hadisi hii ya Victor Hugo, Mufalme ni mupenda wanawake sana na aogopi kama mwanamuke mwenye anamutamania ni bibi wa mutu ao mutoto wa watu. Kikubwa kwake ni kutaka tu kujifurahisha. Triboulet, mutumwa wa Mufalme, eko na kilema mu mukongo. Kazi yake ni kumuchekesha Mufalme. Lakini na yeye pia eko na mutoto wake mwanamuke muzuri sana mwenye alimupataka na marehemu bibi yake. Triboulet anamupenda kupita vitu vyote vya pa dunia na anamuchunga muzuri sana juu asiangukie mu mutego wa Mufalme kama wanawake wengine. Lakini, ujanja wa Triboulet utaweza kweli kukawia siku nyingi? Kwa sababu ya hasira na chuki aliyokuwa nayo kwa Mufalme, Triboulet anatafuta ginsi ya kulipiza kisasi amuue Mufalme aliyefaulu kumnyanyua mutoto wake, Blanche. Mambo itakuwaje? Itawezekana, ao hasira yake itageuka kuwa hasara kwake?

Victor Hugo (1802–1855) alikubalika kuwa mshairi bora wa Ufaransa na mwandishi wa pekee kabisa wa tamthilia, riwaya na insha. Anahesabika kuwa moja wa waandishi maarufu kabisa kutoka Ufaransa. Kazi zake nyingine maarufu ni pamoja na Les Misérables, Notre-Dame de Paris (The Hunchback of Notre-Dame), Les Contemplations na La Légende des siècles.

Katika “Kanuni kwa kuishi maisha ya kisasa”, Lagarce anaeleza matukio katika maisha ya watu na sheria zinazotawala maisha hayo katika kila ngazi muhimu tangu kuzaliwa hadi kufa. Lakini licha ya kuwa ni orodha ya matukio na maelezo yake alikuwa na ujumbe mwingine katika tamthilia hii; kuhusu urasimu unaogeuka kuwa udikteta wa kanuni, na ni jinsi gani tulivyo watumwa wa kanuni.

Jean-Luc Lagarce (1957–1995) “Kanuni kwa kuishi maisha ya kisasa” ni mmoja ya michezo yake ya kuigiza ambayo imemfanya kuwa msanii anayeongoza katika michezo inayoonyeshwa kwenye majukwaa nchini Ufaransa katika miongo ya mwisho ya karne ya ishirini.

Tamthilia mbili za Kifaransa are translations into Kiswahili of two French plays by Victor Hugo (1802-1855), Le Rois s’amuse and Jean Luc Lagarce (1957 – 1995), Les reglès du savoir vivre dans la société moderne. The translations are done in Kiswahili as it is spoken in the Democratic Republic of Congo (DRC), one of Swahili language’s distinct dialects (Kingwana) which is spoken by possibly the second or third largest population of Kiswahili speakers outside Tanzania, where the so-called Kiswahili Sanifu (Standard Swahili) is spoken. The translator, Marcel KALUNGA MWELA-UBI, is a Professor at Lubumbashi and Kalemie Universities in DRC where he teaches Kiswahili among other subjects.

ISBN 9789987081653 | 150 pages | 198 x 129 mm | 2013 | Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania | Paperback

Categories:

Authors

Editors

Document Actions