Personal tools
You are here: Home Books Harusi ya Dogoli

Harusi ya Dogoli

by Athumani Mauya

Dogoli, kijana shababi kutoka kwenye ukoo maarufu anachumbiwa mke na shangazi yake. Mchumba ni Kijakazi. Taratibu zote zinafuatwa na sherehe kubwa ya harusi inaandaliwa. Kama ilivyo katika mila na desturi za watu wa Pwani, harusi haikamiliki hadi jambo moja muhimu sana kutendeka. Kwa mila na desturi Kwa mila na desturi hizo, bwana harusi anapaswa kumuingilia mchumba wake kimwili mbele ya somo yake huku wageni wakisubiri kwa hamu na shauku kubwa jibu la tendo hilo. Muda unawadia na Dogoli na Kijakazi wanapewa chumba. Baada ya kuhaha na kuhangaika mule chumbani kwa muda huku jasho likimmiminika kama mchoma mabiwi ya mkaa, ama kutokana na kitete, ama kuwa si riziki, jogoo lake linashidwa kuwika. Dogoli anashidwa kutimiza tendo la
ndoa; yaani jogoo linashindwa kupanda mtungi.

Sasa kijana akiwa pale chumbani anatweta kwa marefu na mapana. Baada ya muda auonao kama mwaka mzima, taratibu anachukua nguo zake na kuvaa, mgonjwa, kwa aibu isiyo na kifani. Habari zinatapakaa nje kuwa jogoo la Dogoli haliwiki - si matusi, si nyimbo za kejeli, fujo na umbea huku kila mtu akisema lake; yote yalitanda, “Dogoli si riziki; jogoo lake haliwiki, jongoo halipandi mtungi.” Iliyokuwa iwe furaha kubwa kwake na jamaa zake inageuka kuwa huzuni kubwa.

“Ooh! Chaudele wangu, dume langu shababi, baba yangu kuzimu nimekukosea nini? Nimeumbuka mimi jamani; si bure, kuna mkono wa mtu si bure, kuna mkono wa mtu,”

Mama Dogoli amlilia mwanawe kwa uchungu.

Katika muendelezo wa kisa hiki cha kusikitisha Dogoli anakufa katika mazingira ya kutatanisha na anazikwa kwa kufuata mila zao. Baada ya maziko wanakijiji wanaamua kuwatuma wajumbe wawili kwenda ughaibuni kwa waganga wa jadi kubaini sababu ya kifo cha Dogoli.

Dogoli, a young man from a prominent clan engaged wife by her aunt. All procedures are followed by and a large wedding ceremony is being prepared. As in the customs and traditions of the coastal people, one very important thing has to happen during the wedding. In their customs and traditions, the groom should have sex with his fiancee while guests await eagerly and enthusiastically to the answer of that act. The time arrived and the couple is given room. After a long struggle Dogoli fails to fulfill the marriage act; the gossip spreads everywhere on Dogoli's failure. A very mysterious act happens forcing the village to send two members to go abroad for traditional healers to identify the cause of the mystery. The author, through this novel is determined to preserve the traditions and customs of the people of the North Coast of Tanzania for the benefits of the present and future generations.

ISBN 9789987082827 | 138 pages | 203 x 133mm | 2016 | Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania | Paperback

Categories:

Authors

Editors

Document Actions