Personal tools
You are here: Home Books Zawadi ya Ushindi

Zawadi ya Ushindi

by Ben R. Mtobwa

Idd Amini, kiongozi dhalimu kutoka nchi ya Uganda, alipoiteka sehemu ya nchi ya Tanzania na kuangamiza mamia ya watu wasiokuwa na hatia, serikali ya Tanzania iliamua kumkomesha kabla hajatekeleza maafa zaidi. Iliwatuma vijana wake wakapambane naye ili kusalimisha nchi yao.

Sikamona akiwa kijana barubaru aliukubali mwito wa serikali na kuingia vitani kukabiliana na Idd Amin na kikosi chake. Maisha ya Sikamona yalibadilika kabisa baada ya vita hivi. Hata ingawa walifaulu kumkomesha Idd Amin, Sikamona alibaki na makovu mengi yaliyoiharibu sura yake asijione kastahili kuitwa binadamu tena.

Ni yapi yatakayotokea watakapokutana na Rusia? Atapewa ‘Zawadi ya Ushindi’?

ISBN 9789966561565 | 90 pages | 178 x 127 mm | 1984 | East African Educational Publishers, Kenya | Paperback

Categories:

eBook ISBN: 9789966565938

Authors

Editors

Document Actions