Personal tools
You are here: Home Books Vitimbi vya Mama wa Kambo

Vitimbi vya Mama wa Kambo

na hadithi nyingine

by Ally Yusufu Mugenzi

Vitimbi vya Mama wa Kambo, Wivu, Radhi za Wazazi, Ra ki Maluuni, Mchumba Kaka na Adui Mama ni hadithi zinazosawiri jamii alimochipukia mwandishi, au kuishi na kufanya kazi akiwa polisi, mwandishi wa habari na mtangazaji wa redio katika nchi za Tanzania, Rwanda, Burundi na Uingereza kwa takriban miaka 40. Kitabu hiki ni matokeo ya maombi ya watu wengi waliomsikiliza akizisimulia katika kipindi cha Hadithi na Muziki cha Redio Rwanda katika miaka ya 1980 na 1990. Hadithi hizi pia zimekuwa zikitumiwa na wakuza mitaala wa Kiswahili nchini Rwanda shuleni na zimewafurahisha wapenzi wengine wa fasihi nje ya shule.

ISBN 9789987084081 | 162 pages | 198 x 129mm | 2020 | Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania | Paperback

Categories:

Authors

Editors

Document Actions