Personal tools
You are here: Home Books Tutarudi na Roho Zetu?

Tutarudi na Roho Zetu?

by Ben R. Mtobwa

Nchi za mstari wa mbele katika ukombozi kusini mwa Afrika zimetendewa mengi maovu na utawala huu dhalimu... Hata hivyo haikupatikana kutokea tishio zito la kutisha kama hili, ambalo linakaribia kutokea. Tukio la kutatanisha ambalo linawatoa machozi wananchi wa nchi mbalimbali. Wanajitokeza mashujaa kwenda Afrika Kusini, lakini kila aendaye huko hurudi na roho yake.

Inspekta Kombora nchini Tanzania jasho linamtoka. Anawathamini mashujaa wengi lakini anamtambua shujaa mmoja; Joram Kiango. Jambo la kusikitisha ni kwamba sasa hivi, Joram ni mtumiaji mzuri ambaye anatembea kutoka jiji hadi jiji akiwa na yule msichana mzuri Nuru. Juhudi za Kombora kumsihi hazifui dafu. Badala yake Joram anafanya maajabu mengine ambayo yanalichafua jina lake hapa nchini na kote duniani. Wakati huo siku ambayo utawala huo umeweka ili kuachia pigo lao la mwisho inazidi kukaribia. Sasa yamesalia masaa...

ISBN 9789966469410 | 182 pages | 178 x 127 mm | 1984 | East African Educational Publishers, Kenya | Paperback

Categories:

Authors

Editors

Document Actions