Personal tools
You are here: Home Books Nyuma ya Mapazia

Nyuma ya Mapazia

by Ben R. Mtobwa

Tanzania iliingia katika uchaguzi mkuu ulioshirikisha vyama vingi kwa mara ya kwanza mwaka wa 1995. Kampeni kubwa za kitaifa na kimataifa zilifanyika hadharani na sirini. Yako mengi yaliyokuwa yakiendelea ‘Nyuma ya Mapazia’. Mengi ya kutisha na kuogofya, na ambayo yaliambatana na matumizi makubwa ya pesa, mauaji ya kikatili na ujambazi usio na kifani. Joram Kiango, Inspekta Kombora na kikosi kizima cha polisi wanagonga mwamba katika harakati zao za kutatua kizungumkuti hicho. Kutokweka kwa King Halfan King na maiti ya mpenziwe kupatikana ikielea ufukweni wa Bahari ya Hindi kunazidisha maswali mengi bila majibu. Hata hivyo, kizungumkuti hiki kitatatuliwa?

ISBN 9789966561558 | 152 pages | 178 x 127 mm | 1984 | East African Educational Publishers, Kenya | Paperback

Categories:

eBook ISBN: 9789966565921

Authors

Editors

Document Actions