Personal tools
You are here: Home Books Njama

Njama

by E.A. Musiba

Mpelelezi mashuhuri wa Afrika, Mtanzania, Willy Gamba, akiwa likizoni huko Afrika Magharibi, jijini Freetown, Sierra Leone, anatumiwa ujumbe wa haraka arudi upesi nchini kwani kumetokea hujuma kubwa. Kutokana na uzalendo wake hapotezi muda, hima anarejea nchini. Chifu wake anamweleza kuwa shehena kubwa ya silaha za kivita ambazo ni mali ya wapigania uhuru wa kusini mwa Afrika, imeibiwa bandarini katika mazingira ya kutatanisha. Habari hizi zinaleta utata mwingi, baadhi ya nchi zikisema ni njama za Makaburu, na nyingine zikisema ni njama za Tanzania. Katika kiza kinene kinachozunguka suala hili, serikali ya Tanzania inamtuma Willy Gamba kuwasaka majasusi hawa. Hapo ndipo patashika zinaanza na jiji la Dar es Salaam linakumbwa katika wimbi la msukosuko wa uhaini, usaliti, na mauaji ya kikatili...

ISBN 9789987083237 | 194 pages | 198 x 129mm | 2018 | Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania | Paperback

Categories:

Authors

Editors

Document Actions