Personal tools
You are here: Home Books Mirathi ya Hatari

Mirathi ya Hatari

by C.G. Mung'ong'o

Gusto, kijana mdogo wa shule, hakurithi mali ya marehemu baba yake tu, bali pia amerithi tunguri zake, madaraka yake ya kiwanga na mlolongo mzima wa visa, visasi na vinyongo vya baba yake. Urithi huu unamtoa Gusto katika ulimwengu wa wachawi. Hatimaye, baada ya kupambana na vitimbi, hasara na mikasa ya kutisha, inambidi Gusto akate shauri kati ya kuyatekeleza matakwa ya marehemu baba yake na kuyatimiza matakwa ya dhamiri yake binafsi na ya jumuiya yake inayotafuta maendeleo ya kisasa. Mvutano unaotokea unaukiuka uwezo wake alioupata shuleni, na kutisha kumrarua vipande vipande...

Hiki ni kisa cha kutisha na kutaharakisha, kinachotuingiza katika undani wa uganga wa uchawi na mazingaombwe, na hatimaye kutuacha tukijiuliza kama kweli mambo hayo yanayo manufaa yoyote kwa jamii yetu au ni doa na mirathi ya hatari tu katika utamaduni wetu.

Gusto, the little school boy, did not inherit anything material from his father, but did inherit his witchcraft; its power, reprisals and vindictiveness. 

ISBN 9789976102451 | 86 pages | 203 x 127mm | 1977 | Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania | Paperback

Categories:

Authors

Editors

Document Actions