Personal tools
You are here: Home Books DOA

DOA

by Kithaka wa Mberia

Profesa Kithaka wa Mberia anafundisha na kufanya utafiti katika Idara ya Isimu na Lugha, Chuo Kikuu cha Nairobi, Nairobi, Kenya. Mbali na kufundisha na kufanya utafiti, anajishughulisha na uandishi wa mashairi na tamthilia. Tamthilia yake maarufu iitwayo Kifo Kisimani ilikuwa kitabu cha lazima katika mtihani wa kidato cha nne nchini Kenya kuanzia 2006 hadi 2012. Tamthilia yake nyingine iitwayo Natala ilikuwa kitabu cha kutahiniwa katika vyuo vya walimu, pia nchini Kenya, kuanzia 2005 hadi 2016. Mwandishi amewahi kukariri mashairi yake katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na Kenya, Tanzania, Iran, Marekani, US Virgin Islands, United Arab Emirates, Upolanzi, Ujerumani na Italia.

Mbali na Doa, Kifo Kisimani na Natala, Profesa Kithaka wa Mberia amechapisha vitabu vingine ambavyo ni Mchezo wa Karata (mashairi), Bara Jingine (mashairi), Redio na Mwezi (mashairi), Msimu wa Tisa (mashairi), Rangi ya Anga (mashairi) na Maua Kwenye Jua la Asubuhi (tamthilia). Diwani nyingine zake mbili za mashairi, Mvumo wa Helikopta na Bustani ya Miungu (huenda vichwa hivi vikabadilkika), zinatarajiwa kuchapishwa mwaka huu na mwaka ujao mtawalia.

ISBN 9789966794420 | 130 pages | 178 x 127 mm | 2018 | Marimba Publications, Kenya | Paperback

Categories:

Authors

Editors

Document Actions